Hhm, habibi nikuulize swali, kipi cha kukuongeza Kama unaona bado sema kilichopungua Vingine vyote tayari madeko kunidekeza Umeniwezea haapo chali mi ushaniuwa Penzi lako mradi naweza kulikopea Mamlaka yenye kodi watudai na fidia Ah! Maana raha zimezidi paka zanimwagikia Hmm! Maana raha zimezidi paka zanimwagikia Ufukweni Ufukweni mwa bahari (ah! Mikono) Mikono tumeshikana (ah! Mawimbi) Mawimbi yameshamiri (Nyoyo zime!) Nyoyo zimesemezana Kwako nimezama Kwako nimezama Kwako nimezama Kwako nimezama Aah! Upande kanga ukinivalia Kiunoni shanga zinachungulia Ndo ugonjwa wangu, ndo ugonjwa, wa ah! Wala siendi kwa mganga wakaniibia Mama nyakanga nimemrithia Sio shida zangu, sio shida zaa Na ah! Huba lako biriani Lenye shombo shombo ya mbuzi Aiy napenda unavyonisifu laini Ah! Nafaa kwa matumizi Ufukweni Ufukweni mwa bahari (ah! Mikono) Mikono tumeshikana (ah! Mawimbi) Mawimbi yameshamiri (Nyoyo zime!) Nyoyo zimesemezana Kwako nimezama (kwako nimera niko rarara) Kwako nimezama (kwako nime nimezaama) Kwako nimezama (oh nimezaa nimezaama) Kwako nimezama (kwako nime eeeh eeh zama) Hili penzi limemshindwa shetwani mkaa kichwani Mtaliweza nyinyi wapambe wakaa vibarazani Hili penzi limemshindwa shetani mkaa kichwani Mtaliweza nyinyi wapambe wakaa vibarazani