Tunapojituma Kuyaharibu makaazi yetu Tunajihatarisha Bila shaka twajiangamiza Muda wetu wayoyoma Kadri unavyosonga Tunajiteketeza Misitu ikiisha utavutaje mvua Jukumu letu kuelewa Kuwa jua, mwezi, mvua na ardhi Wanyama pori na adinasi Mito, milima, misitu na nyasi Vidudu na ndege wa angani Vimefumwa kwa pamoja Ulimwengu ukizunguka Kile tunachopanda Bila shaka ndicho tutavuna Kama jua likitua Yale tunayofanya Bila shaka yatatufuata Binadamu ni tishio kubwa kwa dunia Na vitendo anavyo fanya Hufanya viumbe kuumia Sasa chukua hatua Wakati ndio sasa Kuyahifadhi mazingira Kupata amani Twahitaji uwiano Kuilinda dunia Kwa vizazi vijavyo Ulimwengu ukizunguka Kile tunachopanda Bila shaka ndicho tutavuna Kama jua likitua Yale tunayofanya Bila shaka yatatufuata